Search This Blog

Sunday, June 23, 2013

UJIO WA RAIS OBAMA TANZANIA WAWATESA MACHINGA NA WAUZA MAGAZETI POSTA

 Na. Issa Gombera

Rais Barack Obama wa Marekani  akisalimiana na Rais  Jakaya  Kikwete alipotembelea nchini Marekani hivi karibuni
Rais Obama
Hali  ilivyo kwa  sasa  eneo la Posta  mpya  jijini Dar es Salaam baada ya wafanyabiashara  ndogo ndogo machinga  na  wauza magazeti na vocha  eneo  hilo  kuondolewa na mgambo  wa  jiji katika zoezi la kusafisha jiji kwa ajili ya ugeni  huo mkubwa nchini

.....................................................

ZIKIWA zimebaki  siku chache kabla  ya  Rais  wa Marekani Barack Obama  kufanya  ziara  yake chini Tanzania ,wafanyabiashara  ndogo ndogo maarufu kama Machinga na  wauza magazeti na  vocha eneo la Posta mpya  jijini Dar es Salaam  wamedai  kunyanyasika na mgambo  wa  jiji kupitia msako mkali unaofanyika .
Msako  huo  umeanza mapema asubuhi ya  leo katika  eneo hilo la Posta na maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ambako msafara wa Rais Obama utapita kutokea  uwanja  wa kimataifa  wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam 

Wakizungumza na mtandao  huu wa www.matukiodaima.com baadhi ya  wafanyabiashara  hao ambao wamelazimika  kusitisha shughuli za biashara  zao  eneo  hilo ,wamesema  kuwa mbali ya ujio  huo  wa Rais Obama nchini  kuwa ni heri kwa Taifa  ila kwa upande  wao wanapinga hatua ya mgambo  kuwanyanyasa kwa  kuwatimua  eneo hilo ambalo  siku  zote  wamekuwa wakifanya kazi na mbaya  zaidi  wameamua kuwatimua hadi  wauza magazeti .

 Alisema mfanyabiashara  Ally Husein  kuwa  kutokana na siku ya  ziara ya Rais Obama  kuwa bado kama  takribani siku 12 mbele  ni  vema uongozi  wa jiji na mkoa  wa Dar es Salaam ukatumia busara  zaidi kwa  kuwaacha kwa  siku hata 7 mbele ama tano  ili  waendelee na biashara kwa ajili ya  kujitafutia mahitaji yao ya  kila  siku kuliko kuwazuia kuanzia leo .

"Kweli  ujio  huu  wa Rais Obama  unatutesa  sana  sisi  walalahoi ambao tunategemea  kuendesha maisha  yetu kwa kuwepo hapa Posta kwa kufanyabiashara za kuuza magazeti na vocha.....Serikali ya mkoa  wa Dar es Salaam tunaomba ilitazame kwa undani  zaidi suala  hili la kutulaza njaa kwa siku zote 12 bila kufanya shughuli"

Hata  hivyo alisema  kuwa  idadi kubwa ya  wafanyabiashara  eneo hilo wamekuwa wakiendesha biashara  zao kwa kupitia mikopo hivyo kuzuiwa kwa muda  wote  huo kutawaharibia mwelekeo  wa kimaisha  .

Hivyo  alishauri  serikali kuwa katika maandalizi ya  ujio  wa Rais  Obama nchini  bado  kutumia njia nzuri ya  kuweka  jiji  safi pasipo kuwaumiza  wananchi  wenye  kipato cha chini wanaofanya  shughuli zao katika eneo hilo.

"Hivi kama  siku  zote  tumekuwa  tukiuza magazeti katika eneo hilo na hakukuwa na uchafuzi  wowote wa mazingira  leo serikali inatuondoa eneo hili na kutuona kama ni uchafu ....kweli katika  hili ni  kutunyanyasa  wanyonge

No comments:

Post a Comment