Search This Blog

Sunday, October 23, 2011

MTOTO MWINGINE WA GADDAFI AUAWA



Serikali ya Libya inasema kuwa mtoto mwanamume wa Kanali Gaddafi, pamoja na wajukuu watatu, waliuwawa katika shambulio la karibuni la ndege za NATO dhidi ya Tripoli.

Msemaji alieleza kuwa kiongozi wa Libya mwenyewe alisalimika katika nyumba hiyo alimokuwa akiishi mwanawe, Saif Al-Arab Gaddafi.
NATO, kwenye taarifa yake, inasema ililenga pahala pa uongozi wa shughuli za kijeshi, haikulenga mtu maalumu, lakini inasikitika kuwa kuna watu walikufa.
Hakuna maiti waliooneshwa lakini shambulio hilo lililenga eneo la makaazi mjini Tripoli.
Serikali inasema watu wane waliuwawa, yaani Saif al-Arab, mtoto mwanamme mdogo kabisa wa Gaddafi, na watoto wa Saif watatu.
Mwaka 1986, Gaddafi alipoteza mtoto wa kike, katika shambulio la ndege za jeshi la Marekani.
Msemaji wa Libya, Moussa Ibrahim, anasema shambulio la jana ni ushahidi wa wazi kuwa sasa kiongozi wa Libya, na familia yake, wanalengwa.
Punde NATO ilitoa taarifa kusema kuwa inaendelea kulenga vituo vya uongozi vya serikali lakini haiwalengi watu fulani.
Msemaji wa serikali, Moussa Ibrahim anadai kuwa Kanali Gaddafi na mkewe walikuwako ndani ya nyumba hiyo wakati wa shambulio hilo, lakini ni shida kuona vipi aliweza kunusurika bila ya kujeruhiwa, katika uharibifu uliosababishwa na makombora matatu yaliyoangushwa papo kwa papo.
Uchina na Urusi katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina wasiwasi kuwa NATO inapindukia idhini ya mwaka 1973.

GADDAFI ALIVYOUAWA

TRIPOLI, Libya
Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha

UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya
waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42.

Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Jinsi alivyouawa

Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti.

Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani.

"Gaddafi alipigwa risasi kichwani," Bw. Mlegta alisema na kuongeza kuwa kulikuwepo na mashambulizi makali dhidi ya wafuasi wake.

Bw. Mlegta aliiambia Reuters kwamba mbali na kupigwa kichwani, Kanali Gaddafi, alikamatwa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili, wakati akijaribu kukimbia na msafara ambao ulishambuliwa na ndege za NATO.

Mauji hayo ambayo yalikuja baada ya kukamatwa, ni miongoni mwa mapinduzi  makubwa zaidi katika ukanda wa nchi za Kiarabu ambayo yalizing'oa tawala za Misri na Tunisia na kutishia usalama wa viongozi wa Syria na Yemen.

Mkuu wa majeshi auawa

Kamanda wa Brigedia ya 11, Bw. Abdul Hakim Al Jalil, alisema kuwa Mkuu wa majeshi ya Kanali Gaddafi, Bw. Abu Bakr Younus Jabr naye aliuawa, na alishuhudia mwili wake.

Pia, Ofisa mwingine wa NTC, alisema kuwa pia Bw. Moussa Ibrahim, msemaji wa Bw. Gaddafi, alikamatwa karibu na mji wa Sirte, alikouawa bosi wake.

"Moussa Ibrahim, vilevile amekamatwa na wote wamepelekwa chumba cha upasuaji," aliongeza.

Hata hivyo, awali Bw. Jamal abu-Shaalah, ambaye ni kamanda mkuu wa  NTC, aliiambia Al Jazeera, kwamba Kanali Gaddafi alikuwa amekamatwa, lakini haikuwa ikifahamiki wazi kama yupo hai ama amekufa, lakini alionekana akipumua.

Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya wapiganaji wa baraza la  NTC,kudaia kukuuteka mji wa alikozaliwa kiongozi huyo Sirte,baada ya wiki moja ya mapigano.

Taarifa zenye utata

Baada ta shambulio hilo taarifa za akila aina zilianza kusambaa, ambapo mmija wa wapiganai vijana, Bw. Mohammed (20) ambaye alikutwa akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka New York Yankees, alisema kuwa Kanali Gaddafi alikutwa akiwa amejificha kwenye shimo ardhini.

Aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kiongozi huyo wa zamani, baada ya kukamatwa aliwaeleza wapiganaji wasimpige risasi.

Mpiganaji huyo wa waasi alisema kuwa baada ya kujeruhiwa alisafirishwa kwa gari la wagonjwa hadi katika mji wa Misrata.

"Alichukuliwa na gari la wagonjwa," alisema mpiganaji huyo. "Allah akbar" (Mungu ni mkubwa), alisema mpiganaji huyo huku akirusha risasi hewani.

Sherehe Tripoli

Mwandishi wa BBC, mjini Tripoli, Bi. Caroline Hawley, alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, milio ya meli na magali ilisikika katika mji huo huku milio ya risasi ikisikika hewani na watu wakishangilia.

"Hakuna vikosi vya Gaddafi tena," Kanali Yunus al-Abdali, aliiambia Reuters. "Kwa sasa tunawafukuza wapiganaji wake ambao wanajaribu kukimbia," aliongeza.

Friday, October 21, 2011


HUU NDIO UKWELI WA SKENDO YA WEMA NA DIAMOND KUACHANA,!!


Habari zilizoenea hivi sasa ni juu ya uvumi wa kuachana kwa waliokuwa wapenzi maarufu na wenye penzi la skendo hapa Tanzania,hapa namzungumzia Wema SEPETU n Naseeb Abdul,ambao kwa sasa inavyosemekana wawili hao wamepeana kibuti na kila mmoja anachukua hamsini zake.Uvumi huo uliibuka baada ya wana na wapenzi wanaochati kupitia BBM kupata sms kutoka kwa mrembo huyo akipigana vijembe na watu tofauti juu ya kuachana kwa wawili hao,huku Wema akionekana kutoa maneno ya kashifa na makali kwa watu mbalimbali ikiwemo waigizaji wenzake.Lakini wote wawili Wema na Diamond walipotafutwa na media tofauti kuzungumzia juu ya swala hilo hawakuwa tayari kutoa ushirikiano na Diamond hakupokea simu kabisa.

Saturday, July 2, 2011

DOGO MWENYE MWILI WACHUMA...

DOGO MWENYE MWILI WACHUMA...

Mtoto mwenye umri wa miaka sita wa nchini Croatia amewashangaza watu duniani kwa mwili wake wenye uwezo wa kunasa vitu mbalimbali vyenye asili ya chuma
Ivan Stoiljkovic ana uwezo wa kunasa hadi kilo 25 za vitu vya chuma kwenye kifua chake na amekuwa kivutio duniani kwa mwili wake wenye sumaku ambao una uwezo wa kunasa sarafu,vijiko,umma,sahani,masufuria na hata simu za mkononi....
Wazazi wake walisema kuwa Ivan anapovua shati lake ana uwezo wa kuvinasa kama sumaku vitu vyovyote vyenye asili ya chuma na pia anadaiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko watoto wa umri wake,mbali na kuwa na umri mdogo wa miaka sita tu ana uwezo wa kubeba kirahisi mfuko wa simenti wa kilo 22 Kali ya yote imedaiwa kuwa Ivan kwa kutumia mikono yake alisaidia kuyaondoa maumivu ya tumbo ya babu yake alipoweka mikono yake juu ya tumbo lake na pia alimsaidia jirani yake aliyekuwa ameumia miguu kwenye ajali ya trekta kwa kumuondolea maumivu yake ya miguu alipoweka mikono yake juu ya miguu yake

ETI....BEN PAUL AJIUNGA NA THT...?!


 

ETI....BEN PAUL AJIUNGA NA THT...?!
Mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa R&B kwenye Kili Music Awards 2011,Ben Paul imefunguliwa kuwa yuko mbioni kujiunga na Kundi la THT...
Ben Paul alichukua tuzo kupitia wimbo wake wa Nikikupata na alifunguka kuwa alikua THT kabla ya kupata offer toka M-Lab chini ya producer Duke na kwa sasa mkataba wake na M-Lab umekwisha baada ya kutoa album moja! ....Na kwa sasa watu waelewe kuwa Ben Paul yuko huru kufanya kazi na mtu yoyote coz hata kwenye album yake artist toka THT wamepata shavu la kufanya naye kazi!....Good Luck ya Kila la kheri

Tuesday, June 28, 2011

WASANII NA WACHEZAJI WA BONGO SHULE MUHIMU

KADIRI siku zinavyozidi kwenda na teknolojia pia inakua; hii inahitaji watu pia kuyamudu mazingira haya ya sayansi na teknolojia.
Nchi zinazoendelea hapa duniani huenda sambamba na kukua kwa sayansi na teknolojia ambayo ndiyo inayofanya dunia kuwa kijiji.
Kukua huku kwa sayansi na teknolojia hapa Tanzania kumeleta mambo hasi na chanya kwa wananchi ambapo kwa watu wenye uelewa finyu huyafanya mambo kuwa hasi.
Katika mtazamo wangu wa leo ningependa kuzungumzia wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii wa fani mbalimbali ambao wamekwishapata majina lakini sasa shule wameamua kuipa kisogo kwa maana ya kujiendeleza kitaaluma na kujikita zaidi katika kucheza mpira na kuigiza.
Pengine nianzie na baadhi ya wachezaji wa soka ambao wameshapata majina kupitia timu mbalimbali za Ligi Kuu ambao wanakipiga wakiwa wametwaliwa katika shule za michezo (sports academies) ambazo zilikuwa zikiwapa elimu ya soka na taaluma nyingine kwa lengo la kuwa na fani nyingi ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini.
Hoja yangu ni kuwa wachezaji hao baada ya kupata majina wamejisahau kujiendeleza kielimu na badala yake wamekalia kucheza soka lakini wakisahau mpira una kupanda na kushuka jambo linaloweza kuwagharimu baadaye kama ilivyowahi kutokea kwa baadhi ya wachezaji.
Nayasema haya nikiwa nimeshuhudia wachezaji hao wakiwa katika hali ngumu za maisha huku namna ya kujiendeleza kielimu ikiwa imefikia ukomo kwa maana ya uwezo wa kujilipia karo huku timu walizokuwa wakizichezea zikiwa zimewaacha na kosa jingine kubwa ambalo hulifanya ni kujisahau kuweka akiba wakiamini nyota yao itaendelea kung’ara milele.
Siyo kwamba wachezaji wote hawana elimu lakini ni wengi wao ambao wana kiwango cha chini cha elimu na wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza mpira kutokana na vipaji vyao lakini baada ya kiwango kushuka hujikuta wakitaabika na kuwa ombaomba wakiwa wametelekezwa na klabu zao.
Kwa mtazamo wangu ni wakati wa wachezaji wa Tanzania iwe wametoka katika shule za michezo au hawakupitia huko kucheza soka huku wakijipambanua na elimu ili kukabiliana na mizengwe ya soka ya Tanzania ambapo wachezaji kuachwa ni suala la kulala na kuamka.
Wachezaji hao hawapaswi kujisahau na kujikita katika soka zaidi badala yake watambue bado wanatakiwa kujipa nafasi ya kusoma ikiwezekana pale wanaposaini mikataba yao na klabu husika kuweka kipengele cha kupata fursa ya kusoma ili kujitengenezea mazingira ya baadaye hata baada ya kustaafu soka.
Lakini hali hii haiwagusi wachezaji peke yake hata wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo ya uigizaji ambayo imekuwa na mashiko kwa jamii katika miaka ya hivi karibuni kujisahau kwao na kulewa na ustaaa waliokwishaupata badala ya kusoma.
Nasema hivi kwa sababu kuna baadhi ya wasanii iwe wa muziki au filamu baada ya kupata majina kupitia kazi zao za sanaa wameamua kuikacha shule na kujikita katika usanii zaidi.
Lakini leo hii kuna hao walioitosa shule na kuona haina umuhimu wamepotea kabisa kwenye ulimwengu wa sanaa na kukosa vyote kwa wakati mmoja.
Ni muhimu kwa wasanii wetu kujifunza kutoka kwa wasanii wa ughaibuni na siyo kuishia kuiga mambo ya laana tu na kuacha vitu vya muhimu ambavyo wasanii wa majuu wanavifanya, hususan katika masuala ya elimu.
Nina uhakika kuna baadhi ya wasanii wa Kibongo wanakosa mikataba yenye fedha kutoka nchi za mbali kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha katika masuala ya sanaa.
Binafsi nimefurahishwa sana na hatua ya meneja wa TipTop connection Babu Tale kuamua kumpeleka Dogo Janja shule, kwa kumlipia gharama zote za shule na mahitaji mengine.
Ni mameneja wachache sana ambao huamua kuwapeleka wasanii wao shule, hii imekaa vizuri sana kwa upande wa babu Tale na ni funzo kwa mameneja wengine.
Dunia ya sasa lazima ikimbizane na watu wenye elimu ili kuweza kuyakabili mazingira ni aibu kwa wasanii kukacha shule.
Nasisitiza hili kwa sababu taifa limekuwa likikosa vitu muhimu kama tuzo au makombe kutoka kwa wasanii ambao wanakuwa wameshiriki mambo mbalimbali katika nchi za wenzetu.
Kinachowafanya wasanii kushindwa kumudu ushindani ni kukosa elimu ya ile sanaa na wapo pia ambao hushindwa kutokana na lugha mbovu ya Kiingereza.
Kikubwa kinachowafanya wasanii kukacha elimu ni kulewa sifa ambazo ni za musimu tu, lakini wapo pia ambao wanastahili kupongezwa kutokana na juhudi zao za kujiendeleza kielimu iwe ni kwenye sanaa au mambo mengine.
Nasema hivi kwa sababu kuna wasanii kama Mr. Blue ambao walipopata majina makubwa wakalewa sifa na kuona shule haina umuhimu, ona sasa wako wapi? Wakiulizwa utasikia bado najipanga ndio majibu yao.
Najua kwa sasa atakuwa anajutia uamuzi wake wa kuitosa shule, kwani kwenye muziki havumi tena kwa sasa angekuwa na taaluma nyingine si angeitumia kujipatia kipato na kumrudishia heshima?
Tuache wivu na chuki, kiukweli Ally Kiba anastahili pongezi kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema kimataifa kutokana na wimbo wa ‘Hands Across the World’ uliotungwa na Robert Kelly au R Kelly.
Katika hili wasanii wanapaswa kujifunza na kuchukua hatua, najua wapo wenye viroho vya wivu lakini kimsingi wanatakiwa kuwa na wivu wa maendeleo na si vinginevyo.
Kwa mtazamo wangu nawaomba wachezaji na wasanii waweze kujiendeleza kielimu kwani inawanyima fursa ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataifa na hivyo kujikosesha tuzo na heshima ambazo zingeweza kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa

Monday, June 27, 2011

Na Mwandishi Wetu
Mshiriki wa Shindano la Big Brother Amplified, Bhoke Egna ambaye hivi karibuni alikumbwa na skendo ya kutoa uroda kwa Ernest wa Uganda, amefichua siri ya namna alivyokutana na ‘shemeji’ yetu huyo.

Bhoke alifichua siri hiyo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na Mwandishi Jacqueline Kibacha wa Jarida la  iMagazine la nchini Uingereza ambapo alisema, uhusiano wao ulianzia siku aliyokwenda Afrika Kusini kwa ajili ya usaili wa kuingia Big Brother.

Alisema kuwa, alipokutana na mshikaji huyo jijini Johannesburg kwa mara ya kwanza kulikuwa na mazingira flani ya kuzimikiana lakini hakuna aliyemwambia mwenzake.

“Mara ya kwanza kukutana naye ni Johannesburg nilipokwenda kwa ajili ya usaili wa Big Brother, kulikuwa na mazingira flani ya kuzimikiana lakini hatukuambiana. Tukaenda ‘out’ kufurahia maisha na tuliporejea kwenye nchini zetu, tuliendelea kuwasiliana, tulikuwa tunapigiana simu na kutumiana sms muda mwingi,” alisema Bhoke.

Alipoulizwa ilikuwaje uhusiano wao ukakua haraka sana walipokuwa mjengoni, Bhoke alisema: “Uhusiano wetu haukukua haraka, kama nilivyosema tulikutana kabla ya kuingia pale kwa hiyo ilikuwa ni suala la kulianzisha upya na kuwepo kwenye nyumba moja kulitufanya kuwa karibu zaidi.”

Akizungumzia namna ndugu zake walivyolichukulia suala lake na Ernest, Bhoke alisema kuwa, familia yake inamjua vizuri na mara nyingi wanajadili mambo ya msingi hivyo wamechukulia poa tu.

“Familia yangu ndiyo mhimili wangu hasa mama yangu, wananijua na tunazungumzia mambo ya msingi mara nyingi. Kwa hiyo uhusiano wangu na familia yangu upo kama ulivyokuwa siku za nyuma na wala hakikubadilika kitu,” alisema mwanadada huyo kwa ung’eng’e uliokwenda shule.

Hivi karibuni, Bhoke alikumbwa na skendo ya kufanya mapenzi na Ernest huku kamera zikiwarekodi hivyo kuufanya ulimwengu mzima kushuhudia malavidavi yao

UZINDUZI WA VODACOM MISS TANZANIA 2011 @ KILIMANJARO KEMPINSKI DAR

Posted on 30 April 2011
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam.



Kampuni ya Vodacom usiku huu imezindua rasmi shindano lake la urembo la Miss Tanzania kwa kipindi cha maka 2011. Pichani meneja udhamini wa kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo. Waliosimama nyuma yake ni baadhi ya warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.



Meneja Udhamini wa Kampuni hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo na hivyo kuonyesha vipaji vyao.”Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini wajitokeze kwa wingi kushiriki katika shindano hili na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu”. Alisema Rwehumbiza



Hawa ni baadhi ya warembo Miss Tanzania ambao walikuwepo katika uzinduzi wa rasmi wa shindano na nembo mpya ya mdhamini wao Kampuni ya simu ya Vodacom waling’ara kwa miaka tofauti na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya dunia .Kutoka kushoto ni Angela Damas Miss Tanzania (2001), Nasreen Karim (Miss Tanzania 2009), Jacqueline Ntuyabaliwe (Miss Tanzania 2000), Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997).



Mbunifu wa mitindo ya mavazi nchini Ally Rhemtullah katika uzinduzi huo.



Mwendesha shughuli MC Jokate Mwegelo akisherehesha.



Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010)

KWA HISANI YA BONGOWEEKEND
Tags , , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News
 

Dida akwaa skendo mpya ya ngono

Na Issa Mnally
MTANGAZAJI wa Redio Times FM ya jijini Dar es Salaam mwenye mbembwe, aliyejivika jina la Dida na kuyaweka kando majina yake ya Khadija Shaib (pichani) amekwaa skendo mpya, safari hii ikihusishwa na ngono na mume wa mtu.

Chanzo chetu makini, kimenasa ishu toka pande za Uarabuni, zenye tuhuma kwamba Dida ameweka moyo wake kwa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Jamal Atinda. Atinda anatajwa kuwahi kuishi Bongo na kupiga mzigo katika Kituo cha Radio Clouds miaka ya nyuma, ambapo inaelezwa kwamba alianza kufaidi penzi la mtangazaji huyo enzi hizo akiwa denti.
Taarifa zilizovuja zinaeleza kwamba, Dida ambaye hivi karibuni amekuwa na vijisafari vingi vya nje, amekuwa akipita pande za Uarabuni kujipumzisha kwa mwanaume huyo, ambaye kwa sasa ana mke na mtoto mmoja.

Inaelezwa na mtoa habari wetu kwamba, licha ya mtangazaji huyo kwenda huko kwa siri, mke wa Atinda alishtukia ishu na kuamua kuanzisha timbwili na hatimaye kusepa kwao.

Maelezo ya watuhumiwa Baada ya stori hii kuvuja na kulifikia gazeti hili, paparazzi wetu alimwendea hewani Dida ambaye alikana kwenda Uarabuni lakini alikiri kutoa penzi kwa kijana huyo.
“Jamani watu wabaya, mbona mambo hayo ya zamani sana, Atinda alikuwa mpenzi wangu enzi hizo nasoma!” Alisema Dida. Risasi lilipomsaka kijana huyo mwenye maskani yake kwenye ‘nchi ya mafuta’ na kuulizwa kama ‘anachakachua’ penzi la Dida alicheka na kusema ilikuwa zamani.

“Mke wangu hakuondoka kwa ajili ya Dida, kuna usaliti alifanya, mimi na Dida tulikuwa zamani lakini kwa sasa hata mawasiliano naye sina,” alisema Atinda.

Sunday, June 26, 2011

Ni kweli ustaa Tanzania haupatikani bila skendo?

 

 Mojawapo ya skendo zilizotamba kwenye magazeti

Vichwa vya habari kwenye magazeti vilivyojaa skendo chafu za wasanii wa filamu wa Tanzania

SEKTA ya filamu katika nchi yoyote ile ni sekta yenye nguvu sana, ikizingatiwa kuwa ina uwezo wa kuchangia kwa kiasi kikubwa mno katika uchumi wowote. Sekta hii ina uwezo mkubwa sana wa kuwa kichocheo cha ukuaji wa maendeleo ya haraka na ya kweli ya taifa ya nchi yoyote kwa kuzingatia utamaduni na saikolojia kwa maendeleo halisi na endelevu.

Ingawa sekta ya filamu ni moja tu kati ya sekta nyingi ndani ya tasnia ya burudani inayosimamia ubunifu, lakini filamu zinaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kushawishi ama kutumika kwa ajili ya kuelimisha au kupotosha mambo katika jamii yoyote.

Tasnia ya burudani na ubunifu inajumuisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya filamu na maigizo, muziki, ulimbwende, mavazi na sanaa zingine za kiufundi, hata hivyo sekta ya filamu ni aina ya sekta inayojipambanua katika kusimamia juhudi za kitaaluma kuhusu uzalishaji na uuzaji wa mawazo katika aina mahsusi ya picha halisi itumikayo kuunganisha mahitaji, matumaini na matarajio ya jamii.

Sinema zinakusudiwa katika kuwapa watu fursa ya kusimulia hadithi zao, na kuwaacha na uhuru wa mawazo kutokana na kuingiliwa na mambo ya kigeni. Kwa hali hii watayarishaji na wasanii wa sinema wa Kitanzania wanapaswa kuishi katika maadili yasiyokinzana na maisha ya jamii na utamaduni.

Kila nikiangalia kwa makini hali halisi ya sekta ya filamu hapa nchini, sioni kama kutakuwa na '
future' yoyote katika tasnia hii endapo mambo yataendelea kuachwa yaende ovyo ovyo kama ilivyo sasa. Ikumbukwe kuwa sekta ya filamu ya Tanzania ni sawa na kinda la ndege linalotegemea mzazi alilishe chakula. Ni kama mtoto anayeanza kutembea, ambaye kila aina ya dosari ni mambo ya kawaida yanayotarajiwa kutokea.

Hata hivyo, katika mazingira ya upatikanaji wa miundombinu ya kimasoko katika kulikuza soko la filamu nchini na kimataifa, Wasanii wa Kitanzania wanastahili kuwa na sifa nzuri katika kuhakikisha kuwa tasnia hii inaaminiwa na watu wote wakiwemo wawekezaji.

Nikiwa mwanaharakati na mdau muhimu sana katika sekta hii, kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijionea vituko hivi na vile kutoka kwa wasanii wetu hasa wanaojiita mastaa, ambao wamediriki kusema kuwa huwezi kuwa maarufu kama huna skendo. Jambo hili linawafanya wasanii wengi katika tasnia hii wasiopenda kujihusisha na kashfa yoyote kukabiliwa na changamoto nyingi za kila siku.

Baadhi ya matatizo haya ni ya asili ya kimataifa, wakati mengine ni ya kipekee kwa jamii mbalimbali.

Miongoni mwa mambo ambayo yamezoeleka sana katika jamii yetu hivi sasa kiasi cha kuzifanya akili zetu kuamini kuwa ni mambo ya kawaida kwa msanii yeyote mwenye umaarufu ni pamoja na kusoma habari zenye kuhusiana na skendo mbalimbali za wasanii wetu. Wasomaji wa magazeti pendwa ambayo wengine hupenda kuyaita ya udaku watakuwa ni mashahidi wa jambo hili, kwani ukifuatilia kwenye magazeti hayo wiki nzima utabaini hili kwa urahisi sana.

Hali hii mara kwa mara imekuwa ikizua malalamiko kwa baadhi ya wasanii wenyewe ambao wamekuwa wakiandikwa kwa mabaya yao wanayoyatenda, na pia hata jamii ambayo imekuwa ikiwafuatilia na kufuatilia habari zao pia. Jambo hili ukilitazama kijuujuu unaweza kuyalaumu magazeti hayo na waandishi wanaowaandika vibaya wasanii kwa kudhani kuwa wanavuka mipaka na kuingilia mambo binafsi, lakini kumbe kuna jambo nyuma ya pazia.

Wasanii karibu wote wa nchi hii, maarufu na hata wasiokuwa maarufu nawafahamu vizuri sana, nimewahi kufanya nao kazi na wengine nimewasaidia kuingia kwenye fani hii ya sanaa ya filamu na maigizo. Ukweli ni kwamba walio wengi huwa wanajipeleka wenyewe kwa waandishi ili waandikwe vibaya kwa dhumuni la 'kutoka kisanii', ndiyo maana wengi wao hata wakiandikwa vipi huwasikii kulalamika au kuchukua hatua zozote. Si hivyo tu, hata pale wasanii hawa wanapohisi kuwa umaarufu wao umeanza kuchuja huwatafuta waandishi wa magazeti hayo ili kuosha nyota!

Wengi wa wanaojiita mastaa wa Bongo waliopata umaarufu kupitia skendo za magazetini huwa hawaijui thamani ya ustaa wao hata pale wanapokuwa tayari maarufu. Hii ni kutokana na skendo zao za ngono mfululizo tunazozisoma magazetini ambazo kwa kweli ni ujinga mtupu!

Inashangaza kuona mtu akitokea kwenye filamu moja au mbili tu, tena kwa kushirikishwa kwenye sehemu ndogo ya sinema hiyo, ataanza kujiita staa na kujiingiza kwenye kujitafutia skendo kwenye magazeti ili asomwe. Ndiyo maana utakuta kila kukicha kunaibuka skendo za aibu kibao!

Mfano ni binti mmoja mwenye asili kama Mmanga ambaye kwa sasa anavuma sana kwa skendo za usagaji kwenye magazeti, ni mwaka jana tu alikuwa akinipigia magoti nimuunganishe aweze kuigiza filamu na wasanii maarufu, siku moja akabahatika kushirikishwa kwenye filamu na mmoja wa wasanii maarufu hapa nchini kwa kupewa sehemu ndogo tu ya kuigiza, eti hivi sasa naye anatembea mabega juu huku akitamba kwenye magazeti kwa kashfa za usagaji, kufumwa na midume usiku na nyingine kibao!

Pia kuna wakati niliwahi kufuatwa na msanii mmoja wa kike (jina nalihifadhi) ambaye wakati huo hakuwa na umaarufu kama alionao sasa, aliyetaka iandikwe skendo yake ya kugombewa na mabwana wawili ambao walikuwa viongozi ndani ya kundi la filamu alilokuwa akifanyia mazoezi. Nilimwelekeza mahali pa kupeleka habari zake huku nikimwambia ukweli kuwa mimi si mwandishi wa kufanya promosheni za aina hiyo, bali mimi ni mchambuzi ambaye naitazama sekta nzima ya filamu, mazuri na changamoto zake na kuihabarisha jamii pasipo kujishughulisha na mambo binafsi ya mtu.

Mifano hai ya wasanii wanaoamini kuwa huwezi kuwa maarufu bila kuibua kashfa iko mingi kiasi kwamba nikianza kuwataja nitajaza kurasa zote za gazeti hili na nisiimalize, japo siyo wasanii wote wanaopenda kuandikwa vibaya kwenye magazeti. Wapo baadhi ya wasanii waliokuwa maarufu sana wakati fulani lakini hawakuwahi kuandikwa vibaya kwenye magazeti, na hawakuwahi kuwafuata waandishi ili wawaandike hata kwa jambo zuri kwani waliamini kuwa kazi zao ndizo zilizokuwa zikiwafanya wajulikane.

Sikatai, wapo baadhi ya wasanii hasa wale wanaolalamika baada ya kuandikwa vibaya kwenye magazeti huwa hawapendi kufuatiliwa katika masuala yao binafsi na kuyaweka kwenye vyombo vya habari, lakini mambo ya kuibuka skendo mbaya kila kukicha yanawafanya hata wasanii wenye maadili mema kuogopa kujitambulisha kwa watu kuwa ni wasanii.

Najua kuwa suala la mapenzi halina mipaka na lingeweza kutokea wakati wowote na kwa mtu yeyote hata kwangu mimi ninayeandika, na kama linatokea kwa wasanii wawili watatu hakuna ubaya wowote, lakini hali ilivyo sasa imekithiri kiasi cha kutia kinyaa.

Utakuta msanii wa kike anajilengesha kwa 'pedeshee' fulani halafu akikubaliwa anamfuata mwandishi wa habari na kumwambia aibue skendo kuhusu uhusiano wake na mtu huyo, tena atamtafutia hata picha. Akishaandikwa gazetini atajifanya kulalamika kuwa waandishi wanamfuatilia maisha yake kwa kuwa yeye ni staa!

Iliwahi kutokea kwa msanii mmoja wa kike aliyetamba sana kwenye magazeti enzi hizo kwa kashfa mbalimbali na baadaye akaingia kwenye ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki maarufu wa bongofleva aliyeamua kumuimba vibaya. Msanii huyu wa kike aliyependa sana kuandikwa vibaya lakini baada ya kuamini kuwa ameshapata ustaa alioutaka hakutaka tena kuandikwa kwa mabaya aliyoyafanya, kiasi cha kujisingizia kunywa sumu.

Pia utakuta msanii wa kiume anaamua kutembeza urijali wake kwa wacheza filamu wa kike karibia wote katika kundi lake akiwa hajali kuwa ipo siku watakuja kujuana, halafu anamfuata mwandishi ili aandike tena ikibidi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti kuwa yeye ni kiwembe!

Ule msemo kuwa “ustaa hauji bila skendo” hauna ukweli wowote, ukijiuliza sana wakati wasanii kama Bishanga, Rich Richie, Waridi, Aisha na wengineo wanavuma walitumia skendo zipi kuwafikisha hapo walipokuwa? Au wasanii kama Lumole Matovolwa (Biggie Poppa), Yusuf Mlela, Kemmi, Monalisa, Natasha na baadhi ya wasanii wa aina yao mbona wamepata umaarufu mkubwa bila kuwa na skendo?

Leo hii imekuwa ni jambo gumu sana kwa wasanii walio wengi endapo utaamua kumwita msanii ukataka kumuandika kwa mazuri yake, kwa kuwa walio wengi wanaamini kuwa mambo mazuri hayawezi kuwafanya watoke.

Thursday, June 16, 2011

DALILI TATU KUWA ANACHOROPOKA NJE

Kwa kawaida kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi hakukosi kutofautiana na matokeo yakutofautiana ni kuzozana, sasa linapojitokeza hilo na kwa bahati mbaya hamjafikia muafaka au mmoja wenu kagoma “kukubali yaishe” au kuwa mjinga ili kutofikia pabaya basi mpenzi wako ambae “anatereza”, anaweza kuibuka na maelezo/sentensi zitakazo ashiria kuwa mnaelekea pande tofauti (ham-elewani) na kama kawaida atakurushia wewe lawama kuwa humuelewi, m-bishi au hata kuwa humheshimu.


Kwa yeye kukusingizia hayo ni wazi kuwa yatakuumiza na kukufanya labda uongeze hasira(hakuna jambo baya kama kusingiziwa jambo) lakini kama nilivyokuonya awali kuwa kukasirika hakuruhusiwi kwani tunachojaribu hapa ni kubadili “mtiririko” au “script” ili kuokoa uhusiano wenu sio.


Maelezo yake yako wazi (kumbuka niliwahi kusema kuwa wanaume most of the time husema kilicho kichwani), sasa hapo anakuambia kuwa uhusiano wenu hauko kama ulivyotakiwa kuwa na anaefanya au kusababisha ni wewe(hata kama ni yeye still atakusukumizia wewe) kwani sote tuna jua kwamba wanawake ndio tunaoweza kurekebisha mambo.....we are mothers, dont forget that!


Sasa ziba/zuia au ondoa hasira zako na anza kuzungumza nae taratibu kwa upendo (kama mama na mwana, yaani jisogeze...mshike panaposjikika namuangalie usoni) na kusema kuwa ungependa nyote wawili muwe kwenye mstari mmoja naje ufanye nini ili kufanikisha hilo. Kisha malizia kwa kusema kuwa utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili kumuelewa na kurudisha heshima kwake.

Jichunguze au chunguza kuna kitu gani kimepungua ndani ya uhusiano wenu ambacho kina mfanya ahisi kuwa heshima haipo baina yenu?, kwanini adhani kuwa hum-elewi? n.k alafu rekebisha hizo hitilafu na mambo yatakuwa poa kabisa kwani kinachomtoanje atakuwa anakipata nyumbani.

Jambo linapojitokeza unapaswa kulizngumzia wakati huo (itakubidi ujifunze kuzuia hasira), sio unaacha siku moja au mbili zinapita alafu unarudi nyuma.....kwa mwanaume itakuwa "unapenda kulalama kila wakati" wakati kwako itakuwa "nilihitaji muda kufikiria na kupanga maneno yangu".

Panua uwezo wako wa kiakili au niseme upeo ili uweze kufikiri haraka na kupangilia maneno cha-chap on spot, suingonjee kesho utakuta mwana sio wako.

Huu ni mwisho wa mfuatano wa jinsi ya kugundua kuwa Mpenzi anatereza/toka nje ya uhusino wenu wa kimapenzi/ndoa.
Endelea kuwepo.

FURAHIA KUNGONOKA BILA KUFIKIA MSHINDO

Furahia kungonoka bila mshindo....inawezekana!

Kama unauzoefu na vilevile unapenda ngono (sio kungonoka na kila mtu, nazungumzia wewe na mpenzi wako mmoja tu unaempenda) unaweza kufurahia "muunganiko" wa mwili wako na wa mpenzi wako hasa kama wote mnajua miili yenu vema, yaani vipele vilipo....pale ukishikwa au kumshika mwenzio ananyegema au kupata raha fulani hivi ya kimapenzi.

Kumbuka kuwa Ngono ni kitendo cha kukutanisha viungo venyu vya uzazi (mwili) na sio kufika kileleni hivyo kufurahia au kupata raha (sio utamu ni raha hehehehe utamu mambo mengine, nitafute nitakuambia) bila kufikia mshindo inawezekana kabisa....by the path ni kutokana na uzoefu wangu.

Unajua kuwa kuna wakati unafanya ngono/mapenzi au niseme mnapelekana kwa muda wa saa nzima na ushehe na hakuna anaefika kileleni lakini wakati hili likifanyika unahisi kufurahia ile hali ya ukaribu, kushikana, papasana, kubadilishana mate/kubusu, kulambana na muunganiko wa viungo venu vinavyopendana kwa dhati ambapo kwa wakati huo wewe na yeye "manavimuvuzisha" nje-ndani au juu-chini au mduara (kukata kiuno) kama sio huku na kule na baadae ndio mmoja anawahi kileleni au manafika wote.....unauzoefu na hili? Unaelewa sasa na zungumzia nini eeh?

Ila tatizo linalojitokeza kwa watu wengi ambalo linaweza kupelekea watu kupinga ninachokisema hapa ni kuwa, unapokuwa nampenzi wako au unapofikiria swala la kufanya ngono akili yako inakuwa "tuned" kwenye "lazima nimfikishe kileleni mpaka akome au aombe radhi".....kwani umeambiwa ni adhabu? au "lazima tufike mara tatu" na matokeo yake mnapo anza kufanya mnakuwa mme-focus kwenye kufika kileleni na sio kufurahia miili yenu.

Kwa wale wanaume ambao Mungu kawa jaalia kwenda mwenzo mrefu na wanajua tofauti ya "sex na love making" ndio wazuri katika hili ikiwa tu kamuandaa mpenzi wake (mwanamke) nampenzi huyo (mwanamke) anajua kujizuia kufika kileleni na hapo nyote wawili mtafurahia tendo bila kufika kileleni mapaka mtakapochoka "kubilingishana" ndio mnajiachia na kufika pamoja au moja baada ya mwingine.

Ikiwa wewe ni mwanamke ambae kwa bahati mbaya huwezi kufika kileleni ukiwa umeingiliwa (uume kuwa ndani) basi hii ndio inakufaa zaidi kama wewe na mpenzi wako mnajua kuchezeana vizuri na kwa ustadi.

Unachotakiwa kufanya ili kufurahia hili ni kujiandaa kiakili, kimwili na vilevile mazingira....

Nitakuja kumalizia hilo nikifika nyumbani,.....wacha nimalizie kutumikia watu hapa!

Oh hey! ile mbinu ya mwisho ya kumfanya jamaa atangaze ndoa ambayo ili-base kwenye Poll itafuata pia, karibu sana

Nini cha kufanya, siku ya kwanza!


"Dinah mi nina swali..kama nakutana mara ya kwanza kimwili na mwanaume what should i do n what should i not do??i would really like to makelove to him coz i believe we both love eachother na tumeanza kuwana kahusiano mwanzo wa mwaka huu but we re both very busy n thought we wanted to do it when we can both enjoy n feel ready.

I want to make it special!!coz we trully adore eachother and get along i don want to blow it!postions i should do??viuno??blow job??im planning it to be at ma place ,have a nice home cooked meal,trying to make ma room tempting beemed light,candles,slow music ,wear kinky knickers u know sort of a thing!!looking forward na comments zenu.thanks"
Jawabu: Asante kwa swali lako na pi anaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kwani nilikuwa likizo. Napenda kwanza ukumbuke au utambue kuwa mwanaume siku zote anapenda au anataka kuwa mtendaji mkuu labda niseme kuwa in-control wakati wote hasa hiyo siku ya kwanza ya kukutanisha miili yenu.
Huitaji kujiandaa sana na badala yake jaribu kuwa wewe (be urself) kisha nenda na "flow", ukijiandaa sana unaweza kumuogopesha asirudi tena au akawa anadai ufanye mandalizi hayo kila siku kwa vile ndio uliyoanzanayo so atataka moto uaki pale-pale, sasa siku ukiamua kuwa romantic si jui ndio utafanyaje hehehehehe usijali.
Siku ya kwanza kwa mwanamke na hata kwake yeye mwanaume ni siku ya kujuana miili yenu, i siku ambayo mtu anaweza asi-notice maandalizi yako kwa vile akili yake yote iko kwenye penzi juu yako na jinsi gani atafurahia ku-share mwili wake na wako.
Kwa maelezo zaidi tafadhali nenda kwenye topics za December na saka inayosema "siku ya kwanza". Wachangiaji wengine shukurani za dhati kwa kumuweka sawa mwenzetu.
Kila la kheri!

SERIKALI:STUDIO YA JK NI KWA AJILI WASANII WALIOIOMBA

Tuesday, March 22, 2011

SERIKALI:STUDIO YA JK NI KWA AJILI YA WASANII WALIOIOMBA


Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit ambayo ndiyo imekabidhiwa studio ya kurekodia muziki (Mastering Studio) na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Said Fella (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vifaa hivyo Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sanaa Bi. Angela Ngowi

Saturday, June 11, 2011

HUYU NDIYE MISS TABATA MWAKA 2011


Vodacom miss Tabata mwaka 2011 Fhaizer Ally akipunga mkono mara baada ya kushinda katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Dar West jijini Dar es salaam kulia ni mshindi wa pili Agosta Mashanga na kushoto ni mshindi wa tatu Godliver Mashamba

Thursday, April 21, 2011

MAVAZI HAYA BALAA TUPU DUH!

Jamani wadau oneni hatari hii ya wanenguaji wa kibongo, ona mavazi haya sasa tuulizane Tanzania bila UKIMWI inawezekana?

FID Q AGEUKA MWANAHARAKATI WA MALARIA KWA WASANII WA MWANZA

Fid Q akiwa kama mmoja wa mabalozi wa maralia alishiriki kwa kiwango kikubwa kuelimisha wana hip hop wa home kutumia sanaa kama sehemu ya darasa kwa umma

WASHINDIWA 'SIKU YA UWEZO' WAKABIDHIWA HAKI YAO

Meneja Udhamini na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akimkabidhi hundi Yuda Joseph mfanyakazi wa dukani eneo la Kinondoni jijini kitita cha shilingi milioni kumi alichojishindia katika promosheni ya siku ya uwezo iliyoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati anayeshuhudia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kahude.

Mhh taratibu baba utapasua hiyo


Rais Jakaya kikwete akionyesha kuenzi  utamaduni kwa kupiga ngoma