Search This Blog

Saturday, July 28, 2012





Look at this pic careful,,,moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.
Hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu…..nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu.
Katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu.

Read more: SIKU CHACHE KABLA HAJAFARIKI, STEVEN KANUMBA ALIANDIKA MANENO HAYA:TAFAKARI - BongoCelebrity 

Sunday, October 23, 2011

MTOTO MWINGINE WA GADDAFI AUAWA



Serikali ya Libya inasema kuwa mtoto mwanamume wa Kanali Gaddafi, pamoja na wajukuu watatu, waliuwawa katika shambulio la karibuni la ndege za NATO dhidi ya Tripoli.

Msemaji alieleza kuwa kiongozi wa Libya mwenyewe alisalimika katika nyumba hiyo alimokuwa akiishi mwanawe, Saif Al-Arab Gaddafi.
NATO, kwenye taarifa yake, inasema ililenga pahala pa uongozi wa shughuli za kijeshi, haikulenga mtu maalumu, lakini inasikitika kuwa kuna watu walikufa.
Hakuna maiti waliooneshwa lakini shambulio hilo lililenga eneo la makaazi mjini Tripoli.
Serikali inasema watu wane waliuwawa, yaani Saif al-Arab, mtoto mwanamme mdogo kabisa wa Gaddafi, na watoto wa Saif watatu.
Mwaka 1986, Gaddafi alipoteza mtoto wa kike, katika shambulio la ndege za jeshi la Marekani.
Msemaji wa Libya, Moussa Ibrahim, anasema shambulio la jana ni ushahidi wa wazi kuwa sasa kiongozi wa Libya, na familia yake, wanalengwa.
Punde NATO ilitoa taarifa kusema kuwa inaendelea kulenga vituo vya uongozi vya serikali lakini haiwalengi watu fulani.
Msemaji wa serikali, Moussa Ibrahim anadai kuwa Kanali Gaddafi na mkewe walikuwako ndani ya nyumba hiyo wakati wa shambulio hilo, lakini ni shida kuona vipi aliweza kunusurika bila ya kujeruhiwa, katika uharibifu uliosababishwa na makombora matatu yaliyoangushwa papo kwa papo.
Uchina na Urusi katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina wasiwasi kuwa NATO inapindukia idhini ya mwaka 1973.

GADDAFI ALIVYOUAWA

TRIPOLI, Libya
Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha

UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya
waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42.

Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Jinsi alivyouawa

Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti.

Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani.

"Gaddafi alipigwa risasi kichwani," Bw. Mlegta alisema na kuongeza kuwa kulikuwepo na mashambulizi makali dhidi ya wafuasi wake.

Bw. Mlegta aliiambia Reuters kwamba mbali na kupigwa kichwani, Kanali Gaddafi, alikamatwa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili, wakati akijaribu kukimbia na msafara ambao ulishambuliwa na ndege za NATO.

Mauji hayo ambayo yalikuja baada ya kukamatwa, ni miongoni mwa mapinduzi  makubwa zaidi katika ukanda wa nchi za Kiarabu ambayo yalizing'oa tawala za Misri na Tunisia na kutishia usalama wa viongozi wa Syria na Yemen.

Mkuu wa majeshi auawa

Kamanda wa Brigedia ya 11, Bw. Abdul Hakim Al Jalil, alisema kuwa Mkuu wa majeshi ya Kanali Gaddafi, Bw. Abu Bakr Younus Jabr naye aliuawa, na alishuhudia mwili wake.

Pia, Ofisa mwingine wa NTC, alisema kuwa pia Bw. Moussa Ibrahim, msemaji wa Bw. Gaddafi, alikamatwa karibu na mji wa Sirte, alikouawa bosi wake.

"Moussa Ibrahim, vilevile amekamatwa na wote wamepelekwa chumba cha upasuaji," aliongeza.

Hata hivyo, awali Bw. Jamal abu-Shaalah, ambaye ni kamanda mkuu wa  NTC, aliiambia Al Jazeera, kwamba Kanali Gaddafi alikuwa amekamatwa, lakini haikuwa ikifahamiki wazi kama yupo hai ama amekufa, lakini alionekana akipumua.

Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya wapiganaji wa baraza la  NTC,kudaia kukuuteka mji wa alikozaliwa kiongozi huyo Sirte,baada ya wiki moja ya mapigano.

Taarifa zenye utata

Baada ta shambulio hilo taarifa za akila aina zilianza kusambaa, ambapo mmija wa wapiganai vijana, Bw. Mohammed (20) ambaye alikutwa akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka New York Yankees, alisema kuwa Kanali Gaddafi alikutwa akiwa amejificha kwenye shimo ardhini.

Aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kiongozi huyo wa zamani, baada ya kukamatwa aliwaeleza wapiganaji wasimpige risasi.

Mpiganaji huyo wa waasi alisema kuwa baada ya kujeruhiwa alisafirishwa kwa gari la wagonjwa hadi katika mji wa Misrata.

"Alichukuliwa na gari la wagonjwa," alisema mpiganaji huyo. "Allah akbar" (Mungu ni mkubwa), alisema mpiganaji huyo huku akirusha risasi hewani.

Sherehe Tripoli

Mwandishi wa BBC, mjini Tripoli, Bi. Caroline Hawley, alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, milio ya meli na magali ilisikika katika mji huo huku milio ya risasi ikisikika hewani na watu wakishangilia.

"Hakuna vikosi vya Gaddafi tena," Kanali Yunus al-Abdali, aliiambia Reuters. "Kwa sasa tunawafukuza wapiganaji wake ambao wanajaribu kukimbia," aliongeza.

Friday, October 21, 2011


HUU NDIO UKWELI WA SKENDO YA WEMA NA DIAMOND KUACHANA,!!


Habari zilizoenea hivi sasa ni juu ya uvumi wa kuachana kwa waliokuwa wapenzi maarufu na wenye penzi la skendo hapa Tanzania,hapa namzungumzia Wema SEPETU n Naseeb Abdul,ambao kwa sasa inavyosemekana wawili hao wamepeana kibuti na kila mmoja anachukua hamsini zake.Uvumi huo uliibuka baada ya wana na wapenzi wanaochati kupitia BBM kupata sms kutoka kwa mrembo huyo akipigana vijembe na watu tofauti juu ya kuachana kwa wawili hao,huku Wema akionekana kutoa maneno ya kashifa na makali kwa watu mbalimbali ikiwemo waigizaji wenzake.Lakini wote wawili Wema na Diamond walipotafutwa na media tofauti kuzungumzia juu ya swala hilo hawakuwa tayari kutoa ushirikiano na Diamond hakupokea simu kabisa.

Saturday, July 2, 2011

DOGO MWENYE MWILI WACHUMA...

DOGO MWENYE MWILI WACHUMA...

Mtoto mwenye umri wa miaka sita wa nchini Croatia amewashangaza watu duniani kwa mwili wake wenye uwezo wa kunasa vitu mbalimbali vyenye asili ya chuma
Ivan Stoiljkovic ana uwezo wa kunasa hadi kilo 25 za vitu vya chuma kwenye kifua chake na amekuwa kivutio duniani kwa mwili wake wenye sumaku ambao una uwezo wa kunasa sarafu,vijiko,umma,sahani,masufuria na hata simu za mkononi....
Wazazi wake walisema kuwa Ivan anapovua shati lake ana uwezo wa kuvinasa kama sumaku vitu vyovyote vyenye asili ya chuma na pia anadaiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko watoto wa umri wake,mbali na kuwa na umri mdogo wa miaka sita tu ana uwezo wa kubeba kirahisi mfuko wa simenti wa kilo 22 Kali ya yote imedaiwa kuwa Ivan kwa kutumia mikono yake alisaidia kuyaondoa maumivu ya tumbo ya babu yake alipoweka mikono yake juu ya tumbo lake na pia alimsaidia jirani yake aliyekuwa ameumia miguu kwenye ajali ya trekta kwa kumuondolea maumivu yake ya miguu alipoweka mikono yake juu ya miguu yake

ETI....BEN PAUL AJIUNGA NA THT...?!


 

ETI....BEN PAUL AJIUNGA NA THT...?!
Mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa R&B kwenye Kili Music Awards 2011,Ben Paul imefunguliwa kuwa yuko mbioni kujiunga na Kundi la THT...
Ben Paul alichukua tuzo kupitia wimbo wake wa Nikikupata na alifunguka kuwa alikua THT kabla ya kupata offer toka M-Lab chini ya producer Duke na kwa sasa mkataba wake na M-Lab umekwisha baada ya kutoa album moja! ....Na kwa sasa watu waelewe kuwa Ben Paul yuko huru kufanya kazi na mtu yoyote coz hata kwenye album yake artist toka THT wamepata shavu la kufanya naye kazi!....Good Luck ya Kila la kheri

Tuesday, June 28, 2011

WASANII NA WACHEZAJI WA BONGO SHULE MUHIMU

KADIRI siku zinavyozidi kwenda na teknolojia pia inakua; hii inahitaji watu pia kuyamudu mazingira haya ya sayansi na teknolojia.
Nchi zinazoendelea hapa duniani huenda sambamba na kukua kwa sayansi na teknolojia ambayo ndiyo inayofanya dunia kuwa kijiji.
Kukua huku kwa sayansi na teknolojia hapa Tanzania kumeleta mambo hasi na chanya kwa wananchi ambapo kwa watu wenye uelewa finyu huyafanya mambo kuwa hasi.
Katika mtazamo wangu wa leo ningependa kuzungumzia wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii wa fani mbalimbali ambao wamekwishapata majina lakini sasa shule wameamua kuipa kisogo kwa maana ya kujiendeleza kitaaluma na kujikita zaidi katika kucheza mpira na kuigiza.
Pengine nianzie na baadhi ya wachezaji wa soka ambao wameshapata majina kupitia timu mbalimbali za Ligi Kuu ambao wanakipiga wakiwa wametwaliwa katika shule za michezo (sports academies) ambazo zilikuwa zikiwapa elimu ya soka na taaluma nyingine kwa lengo la kuwa na fani nyingi ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini.
Hoja yangu ni kuwa wachezaji hao baada ya kupata majina wamejisahau kujiendeleza kielimu na badala yake wamekalia kucheza soka lakini wakisahau mpira una kupanda na kushuka jambo linaloweza kuwagharimu baadaye kama ilivyowahi kutokea kwa baadhi ya wachezaji.
Nayasema haya nikiwa nimeshuhudia wachezaji hao wakiwa katika hali ngumu za maisha huku namna ya kujiendeleza kielimu ikiwa imefikia ukomo kwa maana ya uwezo wa kujilipia karo huku timu walizokuwa wakizichezea zikiwa zimewaacha na kosa jingine kubwa ambalo hulifanya ni kujisahau kuweka akiba wakiamini nyota yao itaendelea kung’ara milele.
Siyo kwamba wachezaji wote hawana elimu lakini ni wengi wao ambao wana kiwango cha chini cha elimu na wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza mpira kutokana na vipaji vyao lakini baada ya kiwango kushuka hujikuta wakitaabika na kuwa ombaomba wakiwa wametelekezwa na klabu zao.
Kwa mtazamo wangu ni wakati wa wachezaji wa Tanzania iwe wametoka katika shule za michezo au hawakupitia huko kucheza soka huku wakijipambanua na elimu ili kukabiliana na mizengwe ya soka ya Tanzania ambapo wachezaji kuachwa ni suala la kulala na kuamka.
Wachezaji hao hawapaswi kujisahau na kujikita katika soka zaidi badala yake watambue bado wanatakiwa kujipa nafasi ya kusoma ikiwezekana pale wanaposaini mikataba yao na klabu husika kuweka kipengele cha kupata fursa ya kusoma ili kujitengenezea mazingira ya baadaye hata baada ya kustaafu soka.
Lakini hali hii haiwagusi wachezaji peke yake hata wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo ya uigizaji ambayo imekuwa na mashiko kwa jamii katika miaka ya hivi karibuni kujisahau kwao na kulewa na ustaaa waliokwishaupata badala ya kusoma.
Nasema hivi kwa sababu kuna baadhi ya wasanii iwe wa muziki au filamu baada ya kupata majina kupitia kazi zao za sanaa wameamua kuikacha shule na kujikita katika usanii zaidi.
Lakini leo hii kuna hao walioitosa shule na kuona haina umuhimu wamepotea kabisa kwenye ulimwengu wa sanaa na kukosa vyote kwa wakati mmoja.
Ni muhimu kwa wasanii wetu kujifunza kutoka kwa wasanii wa ughaibuni na siyo kuishia kuiga mambo ya laana tu na kuacha vitu vya muhimu ambavyo wasanii wa majuu wanavifanya, hususan katika masuala ya elimu.
Nina uhakika kuna baadhi ya wasanii wa Kibongo wanakosa mikataba yenye fedha kutoka nchi za mbali kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha katika masuala ya sanaa.
Binafsi nimefurahishwa sana na hatua ya meneja wa TipTop connection Babu Tale kuamua kumpeleka Dogo Janja shule, kwa kumlipia gharama zote za shule na mahitaji mengine.
Ni mameneja wachache sana ambao huamua kuwapeleka wasanii wao shule, hii imekaa vizuri sana kwa upande wa babu Tale na ni funzo kwa mameneja wengine.
Dunia ya sasa lazima ikimbizane na watu wenye elimu ili kuweza kuyakabili mazingira ni aibu kwa wasanii kukacha shule.
Nasisitiza hili kwa sababu taifa limekuwa likikosa vitu muhimu kama tuzo au makombe kutoka kwa wasanii ambao wanakuwa wameshiriki mambo mbalimbali katika nchi za wenzetu.
Kinachowafanya wasanii kushindwa kumudu ushindani ni kukosa elimu ya ile sanaa na wapo pia ambao hushindwa kutokana na lugha mbovu ya Kiingereza.
Kikubwa kinachowafanya wasanii kukacha elimu ni kulewa sifa ambazo ni za musimu tu, lakini wapo pia ambao wanastahili kupongezwa kutokana na juhudi zao za kujiendeleza kielimu iwe ni kwenye sanaa au mambo mengine.
Nasema hivi kwa sababu kuna wasanii kama Mr. Blue ambao walipopata majina makubwa wakalewa sifa na kuona shule haina umuhimu, ona sasa wako wapi? Wakiulizwa utasikia bado najipanga ndio majibu yao.
Najua kwa sasa atakuwa anajutia uamuzi wake wa kuitosa shule, kwani kwenye muziki havumi tena kwa sasa angekuwa na taaluma nyingine si angeitumia kujipatia kipato na kumrudishia heshima?
Tuache wivu na chuki, kiukweli Ally Kiba anastahili pongezi kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema kimataifa kutokana na wimbo wa ‘Hands Across the World’ uliotungwa na Robert Kelly au R Kelly.
Katika hili wasanii wanapaswa kujifunza na kuchukua hatua, najua wapo wenye viroho vya wivu lakini kimsingi wanatakiwa kuwa na wivu wa maendeleo na si vinginevyo.
Kwa mtazamo wangu nawaomba wachezaji na wasanii waweze kujiendeleza kielimu kwani inawanyima fursa ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataifa na hivyo kujikosesha tuzo na heshima ambazo zingeweza kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa