GADDAFI ALIVYOUAWA
TRIPOLI, Libya
UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya
waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42.
Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye.
Jinsi alivyouawa
Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti.
Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani.
"Gaddafi alipigwa risasi kichwani," Bw. Mlegta alisema na kuongeza kuwa kulikuwepo na mashambulizi makali dhidi ya wafuasi wake.
Bw. Mlegta aliiambia Reuters kwamba mbali na kupigwa kichwani, Kanali Gaddafi, alikamatwa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili, wakati akijaribu kukimbia na msafara ambao ulishambuliwa na ndege za NATO.
Mauji hayo ambayo yalikuja baada ya kukamatwa, ni miongoni mwa mapinduzi makubwa zaidi katika ukanda wa nchi za Kiarabu ambayo yalizing'oa tawala za Misri na Tunisia na kutishia usalama wa viongozi wa Syria na Yemen.
Mkuu wa majeshi auawa
Kamanda wa Brigedia ya 11, Bw. Abdul Hakim Al Jalil, alisema kuwa Mkuu wa majeshi ya Kanali Gaddafi, Bw. Abu Bakr Younus Jabr naye aliuawa, na alishuhudia mwili wake.
Pia, Ofisa mwingine wa NTC, alisema kuwa pia Bw. Moussa Ibrahim, msemaji wa Bw. Gaddafi, alikamatwa karibu na mji wa Sirte, alikouawa bosi wake.
"Moussa Ibrahim, vilevile amekamatwa na wote wamepelekwa chumba cha upasuaji," aliongeza.
Hata hivyo, awali Bw. Jamal abu-Shaalah, ambaye ni kamanda mkuu wa NTC, aliiambia Al Jazeera, kwamba Kanali Gaddafi alikuwa amekamatwa, lakini haikuwa ikifahamiki wazi kama yupo hai ama amekufa, lakini alionekana akipumua.
Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya wapiganaji wa baraza la NTC,kudaia kukuuteka mji wa alikozaliwa kiongozi huyo Sirte,baada ya wiki moja ya mapigano.
Taarifa zenye utata
Baada ta shambulio hilo taarifa za akila aina zilianza kusambaa, ambapo mmija wa wapiganai vijana, Bw. Mohammed (20) ambaye alikutwa akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka New York Yankees, alisema kuwa Kanali Gaddafi alikutwa akiwa amejificha kwenye shimo ardhini.
Aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kiongozi huyo wa zamani, baada ya kukamatwa aliwaeleza wapiganaji wasimpige risasi.
Mpiganaji huyo wa waasi alisema kuwa baada ya kujeruhiwa alisafirishwa kwa gari la wagonjwa hadi katika mji wa Misrata.
"Alichukuliwa na gari la wagonjwa," alisema mpiganaji huyo. "Allah akbar" (Mungu ni mkubwa), alisema mpiganaji huyo huku akirusha risasi hewani.
Sherehe Tripoli
Mwandishi wa BBC, mjini Tripoli, Bi. Caroline Hawley, alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, milio ya meli na magali ilisikika katika mji huo huku milio ya risasi ikisikika hewani na watu wakishangilia.
"Hakuna vikosi vya Gaddafi tena," Kanali Yunus al-Abdali, aliiambia Reuters. "Kwa sasa tunawafukuza wapiganaji wake ambao wanajaribu kukimbia," aliongeza.
Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha |

No comments:
Post a Comment