Na Mwandishi Wetu
Mshiriki wa Shindano la Big Brother Amplified, Bhoke Egna ambaye hivi karibuni alikumbwa na skendo ya kutoa uroda kwa Ernest wa Uganda, amefichua siri ya namna alivyokutana na ‘shemeji’ yetu huyo.
Bhoke alifichua siri hiyo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na Mwandishi Jacqueline Kibacha wa Jarida la iMagazine la nchini Uingereza ambapo alisema, uhusiano wao ulianzia siku aliyokwenda Afrika Kusini kwa ajili ya usaili wa kuingia Big Brother.
Alisema kuwa, alipokutana na mshikaji huyo jijini Johannesburg kwa mara ya kwanza kulikuwa na mazingira flani ya kuzimikiana lakini hakuna aliyemwambia mwenzake.
“Mara ya kwanza kukutana naye ni Johannesburg nilipokwenda kwa ajili ya usaili wa Big Brother, kulikuwa na mazingira flani ya kuzimikiana lakini hatukuambiana. Tukaenda ‘out’ kufurahia maisha na tuliporejea kwenye nchini zetu, tuliendelea kuwasiliana, tulikuwa tunapigiana simu na kutumiana sms muda mwingi,” alisema Bhoke.
Alipoulizwa ilikuwaje uhusiano wao ukakua haraka sana walipokuwa mjengoni, Bhoke alisema: “Uhusiano wetu haukukua haraka, kama nilivyosema tulikutana kabla ya kuingia pale kwa hiyo ilikuwa ni suala la kulianzisha upya na kuwepo kwenye nyumba moja kulitufanya kuwa karibu zaidi.”
Akizungumzia namna ndugu zake walivyolichukulia suala lake na Ernest, Bhoke alisema kuwa, familia yake inamjua vizuri na mara nyingi wanajadili mambo ya msingi hivyo wamechukulia poa tu.
“Familia yangu ndiyo mhimili wangu hasa mama yangu, wananijua na tunazungumzia mambo ya msingi mara nyingi. Kwa hiyo uhusiano wangu na familia yangu upo kama ulivyokuwa siku za nyuma na wala hakikubadilika kitu,” alisema mwanadada huyo kwa ung’eng’e uliokwenda shule.
Hivi karibuni, Bhoke alikumbwa na skendo ya kufanya mapenzi na Ernest huku kamera zikiwarekodi hivyo kuufanya ulimwengu mzima kushuhudia malavidavi yao
No comments:
Post a Comment