Na Issa Mnally
MTANGAZAJI wa Redio Times FM ya jijini Dar es Salaam mwenye mbembwe, aliyejivika jina la Dida na kuyaweka kando majina yake ya Khadija Shaib (pichani) amekwaa skendo mpya, safari hii ikihusishwa na ngono na mume wa mtu.
Chanzo chetu makini, kimenasa ishu toka pande za Uarabuni, zenye tuhuma kwamba Dida ameweka moyo wake kwa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Jamal Atinda. Atinda anatajwa kuwahi kuishi Bongo na kupiga mzigo katika Kituo cha Radio Clouds miaka ya nyuma, ambapo inaelezwa kwamba alianza kufaidi penzi la mtangazaji huyo enzi hizo akiwa denti.
Taarifa zilizovuja zinaeleza kwamba, Dida ambaye hivi karibuni amekuwa na vijisafari vingi vya nje, amekuwa akipita pande za Uarabuni kujipumzisha kwa mwanaume huyo, ambaye kwa sasa ana mke na mtoto mmoja.
Inaelezwa na mtoa habari wetu kwamba, licha ya mtangazaji huyo kwenda huko kwa siri, mke wa Atinda alishtukia ishu na kuamua kuanzisha timbwili na hatimaye kusepa kwao.
Maelezo ya watuhumiwa Baada ya stori hii kuvuja na kulifikia gazeti hili, paparazzi wetu alimwendea hewani Dida ambaye alikana kwenda Uarabuni lakini alikiri kutoa penzi kwa kijana huyo.
“Jamani watu wabaya, mbona mambo hayo ya zamani sana, Atinda alikuwa mpenzi wangu enzi hizo nasoma!” Alisema Dida. Risasi lilipomsaka kijana huyo mwenye maskani yake kwenye ‘nchi ya mafuta’ na kuulizwa kama ‘anachakachua’ penzi la Dida alicheka na kusema ilikuwa zamani.
“Mke wangu hakuondoka kwa ajili ya Dida, kuna usaliti alifanya, mimi na Dida tulikuwa zamani lakini kwa sasa hata mawasiliano naye sina,” alisema Atinda.

No comments:
Post a Comment