.....................................................
ZIKIWA
zimebaki siku chache kabla ya Rais wa Marekani Barack Obama
kufanya ziara yake chini Tanzania ,wafanyabiashara ndogo ndogo
maarufu kama Machinga na wauza magazeti na vocha eneo la Posta mpya
jijini Dar es Salaam wamedai kunyanyasika na mgambo wa jiji kupitia
msako mkali unaofanyika .
Msako huo
umeanza mapema asubuhi ya leo katika eneo hilo la Posta na maeneo
mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ambako msafara wa Rais Obama
utapita kutokea uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius
Nyerere kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam
Wakizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com baadhi ya wafanyabiashara hao
ambao wamelazimika kusitisha shughuli za biashara zao eneo hilo
,wamesema kuwa mbali ya ujio huo wa Rais Obama nchini kuwa ni heri
kwa Taifa ila kwa upande wao wanapinga hatua ya mgambo kuwanyanyasa
kwa kuwatimua eneo hilo ambalo siku zote wamekuwa wakifanya kazi na
mbaya zaidi wameamua kuwatimua hadi wauza magazeti .
Alisema
mfanyabiashara Ally Husein kuwa kutokana na siku ya ziara ya Rais
Obama kuwa bado kama takribani siku 12 mbele ni vema uongozi wa
jiji na mkoa wa Dar es Salaam ukatumia busara zaidi kwa kuwaacha kwa
siku hata 7 mbele ama tano ili waendelee na biashara kwa ajili ya
kujitafutia mahitaji yao ya kila siku kuliko kuwazuia kuanzia leo .
"Kweli
ujio huu wa Rais Obama unatutesa sana sisi walalahoi ambao
tunategemea kuendesha maisha yetu kwa kuwepo hapa Posta kwa
kufanyabiashara za kuuza magazeti na vocha.....Serikali ya mkoa wa Dar
es Salaam tunaomba ilitazame kwa undani zaidi suala hili la kutulaza
njaa kwa siku zote 12 bila kufanya shughuli"
Hata
hivyo alisema kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara eneo hilo
wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa kupitia mikopo hivyo kuzuiwa kwa
muda wote huo kutawaharibia mwelekeo wa kimaisha .
Hivyo
alishauri serikali kuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama
nchini bado kutumia njia nzuri ya kuweka jiji safi pasipo
kuwaumiza wananchi wenye kipato cha chini wanaofanya shughuli zao
katika eneo hilo.
"Hivi
kama siku zote tumekuwa tukiuza magazeti katika eneo hilo na
hakukuwa na uchafuzi wowote wa mazingira leo serikali inatuondoa eneo
hili na kutuona kama ni uchafu ....kweli katika hili ni kutunyanyasa
wanyonge |
No comments:
Post a Comment