MTOTO MWINGINE WA GADDAFI AUAWA
Serikali ya Libya inasema kuwa mtoto mwanamume wa Kanali Gaddafi, pamoja na wajukuu watatu, waliuwawa katika shambulio la karibuni la ndege za NATO dhidi ya Tripoli.
Msemaji alieleza kuwa kiongozi wa Libya mwenyewe alisalimika katika nyumba hiyo alimokuwa akiishi mwanawe, Saif Al-Arab Gaddafi.
NATO, kwenye taarifa yake, inasema ililenga pahala pa uongozi wa shughuli za kijeshi, haikulenga mtu maalumu, lakini inasikitika kuwa kuna watu walikufa.
Hakuna maiti waliooneshwa lakini shambulio hilo lililenga eneo la makaazi mjini Tripoli.
Serikali inasema watu wane waliuwawa, yaani Saif al-Arab, mtoto mwanamme mdogo kabisa wa Gaddafi, na watoto wa Saif watatu.
Mwaka 1986, Gaddafi alipoteza mtoto wa kike, katika shambulio la ndege za jeshi la Marekani.
Msemaji wa Libya, Moussa Ibrahim, anasema shambulio la jana ni ushahidi wa wazi kuwa sasa kiongozi wa Libya, na familia yake, wanalengwa.
Punde NATO ilitoa taarifa kusema kuwa inaendelea kulenga vituo vya uongozi vya serikali lakini haiwalengi watu fulani.
Msemaji wa serikali, Moussa Ibrahim anadai kuwa Kanali Gaddafi na mkewe walikuwako ndani ya nyumba hiyo wakati wa shambulio hilo, lakini ni shida kuona vipi aliweza kunusurika bila ya kujeruhiwa, katika uharibifu uliosababishwa na makombora matatu yaliyoangushwa papo kwa papo.
Uchina na Urusi katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina wasiwasi kuwa NATO inapindukia idhini ya mwaka 1973.