Tembelea blog hii uweze kupata habari mbalimbali zilizochambuliwa kwa kina na wachambuzi wetu,pia unaweza kujiunga na blog kwa kubonyesha link iliyo upande wa kushoto iliyoandikwa followers. Andika habari uitafutayo katika box hapo chini kisha bonyeza search kama hakuna matokeo bonyeza THE WEB kisha soma habari uitakayo
Search This Blog
Saturday, July 2, 2011
DOGO MWENYE MWILI WACHUMA...
Mtoto mwenye umri wa miaka sita wa nchini Croatia amewashangaza watu duniani kwa mwili wake wenye uwezo wa kunasa vitu mbalimbali vyenye asili ya chuma
Ivan Stoiljkovic ana uwezo wa kunasa hadi kilo 25 za vitu vya chuma kwenye kifua chake na amekuwa kivutio duniani kwa mwili wake wenye sumaku ambao una uwezo wa kunasa sarafu,vijiko,umma,sahani,masufuria na hata simu za mkononi....
Wazazi wake walisema kuwa Ivan anapovua shati lake ana uwezo wa kuvinasa kama sumaku vitu vyovyote vyenye asili ya chuma na pia anadaiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko watoto wa umri wake,mbali na kuwa na umri mdogo wa miaka sita tu ana uwezo wa kubeba kirahisi mfuko wa simenti wa kilo 22 Kali ya yote imedaiwa kuwa Ivan kwa kutumia mikono yake alisaidia kuyaondoa maumivu ya tumbo ya babu yake alipoweka mikono yake juu ya tumbo lake na pia alimsaidia jirani yake aliyekuwa ameumia miguu kwenye ajali ya trekta kwa kumuondolea maumivu yake ya miguu alipoweka mikono yake juu ya miguu yake
ETI....BEN PAUL AJIUNGA NA THT...?!
Mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa R&B kwenye Kili Music Awards 2011,Ben Paul imefunguliwa kuwa yuko mbioni kujiunga na Kundi la THT...
Ben Paul alichukua tuzo kupitia wimbo wake wa Nikikupata na alifunguka kuwa alikua THT kabla ya kupata offer toka M-Lab chini ya producer Duke na kwa sasa mkataba wake na M-Lab umekwisha baada ya kutoa album moja! ....Na kwa sasa watu waelewe kuwa Ben Paul yuko huru kufanya kazi na mtu yoyote coz hata kwenye album yake artist toka THT wamepata shavu la kufanya naye kazi!....Good Luck ya Kila la kheri
Subscribe to:
Posts (Atom)