Search This Blog

Sunday, October 23, 2011

MTOTO MWINGINE WA GADDAFI AUAWA



Serikali ya Libya inasema kuwa mtoto mwanamume wa Kanali Gaddafi, pamoja na wajukuu watatu, waliuwawa katika shambulio la karibuni la ndege za NATO dhidi ya Tripoli.

Msemaji alieleza kuwa kiongozi wa Libya mwenyewe alisalimika katika nyumba hiyo alimokuwa akiishi mwanawe, Saif Al-Arab Gaddafi.
NATO, kwenye taarifa yake, inasema ililenga pahala pa uongozi wa shughuli za kijeshi, haikulenga mtu maalumu, lakini inasikitika kuwa kuna watu walikufa.
Hakuna maiti waliooneshwa lakini shambulio hilo lililenga eneo la makaazi mjini Tripoli.
Serikali inasema watu wane waliuwawa, yaani Saif al-Arab, mtoto mwanamme mdogo kabisa wa Gaddafi, na watoto wa Saif watatu.
Mwaka 1986, Gaddafi alipoteza mtoto wa kike, katika shambulio la ndege za jeshi la Marekani.
Msemaji wa Libya, Moussa Ibrahim, anasema shambulio la jana ni ushahidi wa wazi kuwa sasa kiongozi wa Libya, na familia yake, wanalengwa.
Punde NATO ilitoa taarifa kusema kuwa inaendelea kulenga vituo vya uongozi vya serikali lakini haiwalengi watu fulani.
Msemaji wa serikali, Moussa Ibrahim anadai kuwa Kanali Gaddafi na mkewe walikuwako ndani ya nyumba hiyo wakati wa shambulio hilo, lakini ni shida kuona vipi aliweza kunusurika bila ya kujeruhiwa, katika uharibifu uliosababishwa na makombora matatu yaliyoangushwa papo kwa papo.
Uchina na Urusi katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina wasiwasi kuwa NATO inapindukia idhini ya mwaka 1973.

GADDAFI ALIVYOUAWA

TRIPOLI, Libya
Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha

UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya
waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42.

Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Jinsi alivyouawa

Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti.

Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani.

"Gaddafi alipigwa risasi kichwani," Bw. Mlegta alisema na kuongeza kuwa kulikuwepo na mashambulizi makali dhidi ya wafuasi wake.

Bw. Mlegta aliiambia Reuters kwamba mbali na kupigwa kichwani, Kanali Gaddafi, alikamatwa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili, wakati akijaribu kukimbia na msafara ambao ulishambuliwa na ndege za NATO.

Mauji hayo ambayo yalikuja baada ya kukamatwa, ni miongoni mwa mapinduzi  makubwa zaidi katika ukanda wa nchi za Kiarabu ambayo yalizing'oa tawala za Misri na Tunisia na kutishia usalama wa viongozi wa Syria na Yemen.

Mkuu wa majeshi auawa

Kamanda wa Brigedia ya 11, Bw. Abdul Hakim Al Jalil, alisema kuwa Mkuu wa majeshi ya Kanali Gaddafi, Bw. Abu Bakr Younus Jabr naye aliuawa, na alishuhudia mwili wake.

Pia, Ofisa mwingine wa NTC, alisema kuwa pia Bw. Moussa Ibrahim, msemaji wa Bw. Gaddafi, alikamatwa karibu na mji wa Sirte, alikouawa bosi wake.

"Moussa Ibrahim, vilevile amekamatwa na wote wamepelekwa chumba cha upasuaji," aliongeza.

Hata hivyo, awali Bw. Jamal abu-Shaalah, ambaye ni kamanda mkuu wa  NTC, aliiambia Al Jazeera, kwamba Kanali Gaddafi alikuwa amekamatwa, lakini haikuwa ikifahamiki wazi kama yupo hai ama amekufa, lakini alionekana akipumua.

Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya wapiganaji wa baraza la  NTC,kudaia kukuuteka mji wa alikozaliwa kiongozi huyo Sirte,baada ya wiki moja ya mapigano.

Taarifa zenye utata

Baada ta shambulio hilo taarifa za akila aina zilianza kusambaa, ambapo mmija wa wapiganai vijana, Bw. Mohammed (20) ambaye alikutwa akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka New York Yankees, alisema kuwa Kanali Gaddafi alikutwa akiwa amejificha kwenye shimo ardhini.

Aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kiongozi huyo wa zamani, baada ya kukamatwa aliwaeleza wapiganaji wasimpige risasi.

Mpiganaji huyo wa waasi alisema kuwa baada ya kujeruhiwa alisafirishwa kwa gari la wagonjwa hadi katika mji wa Misrata.

"Alichukuliwa na gari la wagonjwa," alisema mpiganaji huyo. "Allah akbar" (Mungu ni mkubwa), alisema mpiganaji huyo huku akirusha risasi hewani.

Sherehe Tripoli

Mwandishi wa BBC, mjini Tripoli, Bi. Caroline Hawley, alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, milio ya meli na magali ilisikika katika mji huo huku milio ya risasi ikisikika hewani na watu wakishangilia.

"Hakuna vikosi vya Gaddafi tena," Kanali Yunus al-Abdali, aliiambia Reuters. "Kwa sasa tunawafukuza wapiganaji wake ambao wanajaribu kukimbia," aliongeza.

Friday, October 21, 2011


HUU NDIO UKWELI WA SKENDO YA WEMA NA DIAMOND KUACHANA,!!


Habari zilizoenea hivi sasa ni juu ya uvumi wa kuachana kwa waliokuwa wapenzi maarufu na wenye penzi la skendo hapa Tanzania,hapa namzungumzia Wema SEPETU n Naseeb Abdul,ambao kwa sasa inavyosemekana wawili hao wamepeana kibuti na kila mmoja anachukua hamsini zake.Uvumi huo uliibuka baada ya wana na wapenzi wanaochati kupitia BBM kupata sms kutoka kwa mrembo huyo akipigana vijembe na watu tofauti juu ya kuachana kwa wawili hao,huku Wema akionekana kutoa maneno ya kashifa na makali kwa watu mbalimbali ikiwemo waigizaji wenzake.Lakini wote wawili Wema na Diamond walipotafutwa na media tofauti kuzungumzia juu ya swala hilo hawakuwa tayari kutoa ushirikiano na Diamond hakupokea simu kabisa.