Search This Blog

Monday, June 27, 2011

UZINDUZI WA VODACOM MISS TANZANIA 2011 @ KILIMANJARO KEMPINSKI DAR

Posted on 30 April 2011
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam.



Kampuni ya Vodacom usiku huu imezindua rasmi shindano lake la urembo la Miss Tanzania kwa kipindi cha maka 2011. Pichani meneja udhamini wa kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo. Waliosimama nyuma yake ni baadhi ya warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.



Meneja Udhamini wa Kampuni hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo na hivyo kuonyesha vipaji vyao.”Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini wajitokeze kwa wingi kushiriki katika shindano hili na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu”. Alisema Rwehumbiza



Hawa ni baadhi ya warembo Miss Tanzania ambao walikuwepo katika uzinduzi wa rasmi wa shindano na nembo mpya ya mdhamini wao Kampuni ya simu ya Vodacom waling’ara kwa miaka tofauti na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya dunia .Kutoka kushoto ni Angela Damas Miss Tanzania (2001), Nasreen Karim (Miss Tanzania 2009), Jacqueline Ntuyabaliwe (Miss Tanzania 2000), Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997).



Mbunifu wa mitindo ya mavazi nchini Ally Rhemtullah katika uzinduzi huo.



Mwendesha shughuli MC Jokate Mwegelo akisherehesha.



Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010)

KWA HISANI YA BONGOWEEKEND
Tags , , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News
 

No comments:

Post a Comment