Search This Blog

Thursday, June 16, 2011

DALILI TATU KUWA ANACHOROPOKA NJE

Kwa kawaida kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi hakukosi kutofautiana na matokeo yakutofautiana ni kuzozana, sasa linapojitokeza hilo na kwa bahati mbaya hamjafikia muafaka au mmoja wenu kagoma “kukubali yaishe” au kuwa mjinga ili kutofikia pabaya basi mpenzi wako ambae “anatereza”, anaweza kuibuka na maelezo/sentensi zitakazo ashiria kuwa mnaelekea pande tofauti (ham-elewani) na kama kawaida atakurushia wewe lawama kuwa humuelewi, m-bishi au hata kuwa humheshimu.


Kwa yeye kukusingizia hayo ni wazi kuwa yatakuumiza na kukufanya labda uongeze hasira(hakuna jambo baya kama kusingiziwa jambo) lakini kama nilivyokuonya awali kuwa kukasirika hakuruhusiwi kwani tunachojaribu hapa ni kubadili “mtiririko” au “script” ili kuokoa uhusiano wenu sio.


Maelezo yake yako wazi (kumbuka niliwahi kusema kuwa wanaume most of the time husema kilicho kichwani), sasa hapo anakuambia kuwa uhusiano wenu hauko kama ulivyotakiwa kuwa na anaefanya au kusababisha ni wewe(hata kama ni yeye still atakusukumizia wewe) kwani sote tuna jua kwamba wanawake ndio tunaoweza kurekebisha mambo.....we are mothers, dont forget that!


Sasa ziba/zuia au ondoa hasira zako na anza kuzungumza nae taratibu kwa upendo (kama mama na mwana, yaani jisogeze...mshike panaposjikika namuangalie usoni) na kusema kuwa ungependa nyote wawili muwe kwenye mstari mmoja naje ufanye nini ili kufanikisha hilo. Kisha malizia kwa kusema kuwa utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili kumuelewa na kurudisha heshima kwake.

Jichunguze au chunguza kuna kitu gani kimepungua ndani ya uhusiano wenu ambacho kina mfanya ahisi kuwa heshima haipo baina yenu?, kwanini adhani kuwa hum-elewi? n.k alafu rekebisha hizo hitilafu na mambo yatakuwa poa kabisa kwani kinachomtoanje atakuwa anakipata nyumbani.

Jambo linapojitokeza unapaswa kulizngumzia wakati huo (itakubidi ujifunze kuzuia hasira), sio unaacha siku moja au mbili zinapita alafu unarudi nyuma.....kwa mwanaume itakuwa "unapenda kulalama kila wakati" wakati kwako itakuwa "nilihitaji muda kufikiria na kupanga maneno yangu".

Panua uwezo wako wa kiakili au niseme upeo ili uweze kufikiri haraka na kupangilia maneno cha-chap on spot, suingonjee kesho utakuta mwana sio wako.

Huu ni mwisho wa mfuatano wa jinsi ya kugundua kuwa Mpenzi anatereza/toka nje ya uhusino wenu wa kimapenzi/ndoa.
Endelea kuwepo.

No comments:

Post a Comment